• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 09, 2019

  BODI YA LIGI YAAHIRISHA MECHI KATI YA MBEYA CITY DHIDI YA YANGA SC SEPTEMBA 18 SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BODI ya Ligi imeufuta mchezo kati ya Mbeya City na Yanga SC uliokuwa uchezwe Septemba 18 mjini Mbeya ili kuwapa fursa ya maandalizi mazuri ya mchezo wa marudiano na Zesco United, Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Septemba 27 mjini Ndola, Zambia.
  Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo imesema kwamba mchezo sasa utapangiwa tarehe nyingine, ili Yanga wapate nafasi pana ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Zesco United.
  Yanga SC wameweka kambi mjini Mwanza kujiandaa na mchezo wa kwanza na Zesco United utakaofanyika Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

  Na juzi walicheza mechi ya kirafiki na kutoa sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji, Pamba Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo, wenyeji wakitangulia kwa bao la Saad Kipanga kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake mpya David Molinga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Kesho Yanga watacheza mechi ya mwisho ya kujipima kwenye kambi yao ya Mwanza kwa kumenyana na Toto Africans hapo hapo Kirumba kabla ya kupanda ndege kurejea Dar es Salaam tayari kuwakabili Zesco United.
  Tayari Yanga wametaja viingilio vya mechi dhidi ya Zesco Jumamosi Uwanja wa Taifa ambavyo ni Sh 100,000 kwa eneo maalum lililopewa jina Royal, Sh. 25,000 kwa VIP A, Sh. 10,000 VIP B na C na 3,000 kwa maeneo ya Orange, Blue na Green.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BODI YA LIGI YAAHIRISHA MECHI KATI YA MBEYA CITY DHIDI YA YANGA SC SEPTEMBA 18 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top