• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 23, 2018

  YANGA SC KUIFUATA MAJI MAJI KWA NDEGE KESHO AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION
  Februari 21, 2018
  Njombe Mji 1-1 Mbao FC (Penalti 6-5)
  Februari 24, 2018
  Singida United v Polisi Tanzania Saa 10:00 jioni
  KMC v Azam FC Saa 1:00 usiku
  Februari 25, 2018
  Maji Maji  v Yanga SC Saa 10:00 jioni
  Buseresere v Mtibwa Sugar Saa 8:00 mchana
  Februari 26, 2018
  Kiluvya United v Tanzania Prisons          Saa 8:00 mchana 
  Stand United v Dodoma FC Saa 10:00 jioni
  Yanga watssafiri kwa ndege kesho kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ASFC dhidi ya Maji Maji  

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kimerejea Dar es Salaam usiku wa jana kutoka Mahe, Shelisheli ambako katikati ya wiki kilikata tiketi ya kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji, Saint Louis Suns United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Uwanja wa Linite.
  Mabingwa hao wa Tanzania wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la kiungo Juma Mahadhi aliyekosekana uwanjani Jumatano kwa sababu ya homa.
  Yanga leo watafanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, kilichopo Kurasini mjini Dar es Salaam kabla ya mapema kesho kusafiri kwa ndege kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili. 
  Kwa kuitoa St Louis, Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo nayo iliitoa El Merreikh ya Sudan.
  Yanga SC wataikaribisha Township Rollers ya Botswana Machi 7 Uwanja wa Taifa, kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi 17.
  Hatua ya 16 Bora ya ASFC itaendelea kesho kwa Singida United kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na KMC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mbali na Maji Maji na Yanga, mechi nyingine za Jumapili ni Buseresere FC watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na JKT Tanzania watakaomenyana na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
  Mechi za 16 Bora ya ASFC zitakamilishwa Jumatatu ya Februari 26, Kiluvya United wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Stand United watakuwa wenyeji wa Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC KUIFUATA MAJI MAJI KWA NDEGE KESHO AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top