• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 19, 2018

  RUVU SHOOTING WAIBAMIZA MTIBWA SUGAR 2-1 MANUNGU, PRISONS YAIPIGA 1-0 MWADUI SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo.
  Hata hivyo, haukuwa ushindi mwepesi, kwani Ruvu walilazmika kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi huo kipindi cha pili.
  Wenyeji, Mtibwa walio chini ya kocha Zuberi Katwila mchezaji wao wa zamani, walitangulia kwa bao la Ismail Aidan dakika ya 40, kabla ya Ruvu kuzinduka na kupata mabao mawili kupitia kwa Baraka Mtuwi dakika ya 45 na Issa Kanduru dakika ya 76.  
  Ruvu Shooting imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Manungu leo

  Ushindi huo unaifanya Ruvu ifikishe pointi 23 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, wakati Mtibwa Sugar inashuka kwa nafasi moja hadi ya sita ikibaki na pointi zake 27 za mechi 19 pia.  
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Tanzania Prisons wametumia vizuri fursa ya kucheza nyumbani kwa kuibamiza 1-0 Mwadui FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, bao pekee la Laurian Mpalile dakika ya 54.
  Prisons nayo inatimiza pointi 29 baada ya ushindi huo katika mechi ya 19 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tano ilipokuwa Mtibwa, sasa ikiwa nyuma ya Singida United yenye pointi 34, Azam FC 35, Yanga 37 na Simba SC 42.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING WAIBAMIZA MTIBWA SUGAR 2-1 MANUNGU, PRISONS YAIPIGA 1-0 MWADUI SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top