• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 20, 2018

  EL HILAL VITANI LIGI YA MABINGWA AFRIKA LEO IKITOKA KULALA 1-0

  TIMU ya El Hilal ya Sudan leo itakuwa nyumbani kuwakaribisha LISCR ya Liberia katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Hilal, moja ya timu zenye historia katika michuani ya klabu barani Afrika, itaingia kwenye mchezo wa leo ikikabiliwa na shughuli ya kupindua matokeo, baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Liberia.
  Jumla ya mechi tatu za marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa wa Afrika zinachezwa leo, nyingine ni kati ya wenyeji, Williamsville AC ya Ivory Coast na Stade Malien ya Mali ambazo mechi ya kwanza zilifungana 1-1 na Olympic de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) itawakaribisha ES Setif ya Algeria walioshinda 6-0 kwenye mechi ya kwanza.
  El Hilal ya Sudan itakuwa nyumbani  leo kuwakaribisha LISCR ya Liberia

  Mechi zaidi za marudiano zitachezwa kesho, zikiwemo kati ya Saint Louis ya Shelisheli na Yanga SC ya Tanzania na El Merreikh ya Sudan na Township Rollers ya Botswana, ambazo washindi wake wa jumla watakutana katika hatua ifuatayo.
  Yanga ilishinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza, wakati Township Rollers ilishinda 3-0 nyumbani pia.
  Saint Louis watakuwa wenyeji wa Yanga SC ya Tanzania nchini ya Shelisheli kesho

  MARUDIANO MCHUJO LIGI YA MABINGWA AFRIKA
  Jumanne Februari 20, 2018
  El Hilal (Sudan) vs LISCR (Liberia) (0-1)
  Williamsville AC (Ivory Coast) vs Stade Malien (Mali) (1-1)
  Olympic de Bangui (CAR) vs ES Setif (Algeria) (0-6)
  Jumatano Februari 21, 2018
  KCCA (Uganda) vs CNaPs Sport (Madagascar) (1-2)
  Mbabane Swallows (Swaziland) vs Bantu (Lesotho) (4-2)
  Aduana (Ghana) vs El Tahadi (Libya) (0-1)
  Mounana (Gabon) vs RC Kadiogo (Burkina Faso) (0-1)
  MFM (Nigeria) vs AS Real (Mali) (1-1)
  MC Alger (Algeria) vs AS Otoho (Kongo) (0-2)
  Horoya (Guinea) vs AS FAN (Niger) (3-1)
  Makkassa (Misri) vs Generation Foot (Senegal) (0-2)
  Saint Louis (Shelisheli) vs Yanga SC (Tanzania) (0-1)
  El Merreikh (Sudan) vs Township Rollers (Botswana) (0-3)
  Leones Vegatarianos (Equatorial Guinea) vs Gor Mahia (Kenya) (0-2)
  Esperance (Tunisia) vs Concorde (Mauritania) (1-1)
  Eding Sport (Cameroon) vs Plateau United (Nigeria) (0-3)
  AS Port (Togo) vs AC Leopards (Kongo) (1-2)
  Zesco (Zambia) vs JKU (Zanzibar) (0-0)
  ASEC Mimosas (Ivory Coast) vs Buffles (Benin) (1-1)
  UD Songo (Msumbiji) vs Ngaya (Comoro) (1-1)
  Be Forward (Malawi) vs AS Vita (DRC) (0-4)
  FC Platinum (Zimbabwe) vs Primeiro de Agosto (Angola) (0-3)
  Pamplemousses (Mauritius) vs Bidvest (Afrika Kusini) (0-2)
  Difaa El Jadida (Morocco) 10-0 Benfica (Guinea Bissau)
  Benfica (Guinea Bissau) vs Difaa El Jadida (Morocco) (0-10)
  Lydia Academic (Burundi) vs Rayon Sports (Rwanda) (1-1)
  Saturday, 24 February 2018
  Armed Forces (Gambia) vs Zanaco (Zambia) (0-3)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EL HILAL VITANI LIGI YA MABINGWA AFRIKA LEO IKITOKA KULALA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top