• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 27, 2018

  WARUNDI KUICHEZESHA YANGA DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
  Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka
  Nyota wa Yanga SC, Emmanuel Martin (kushoto) na Gardel Michael (kulia) ni tumaini la ushindi dhidi ya Township Rollers
  Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

  Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
  Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WARUNDI KUICHEZESHA YANGA DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top