• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 19, 2018

  BAFETIMBI GOMIS AZIMIA UWANJANI AKIICHEZEA GALATASARAY UTURUKI

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Swansea, Bafetimbi Gomis jana alizimia uwanjani wakati wa mechi kati ya timu yake ya sasa, Galatasaray dhidi ya wenyeji Kasimpasa walioshinda 2-1 katika Ligi ya Uturuki.
  Gomis alipoteza fahamu, lakini akaruhusiwa kuendelea na mchezo baada ya kuzinduka.
  Tukio hilo lilitokea dakika ya saba ya mchezo, baada ya Gomis kuinama kushika magoti yake kabla ya kuanguka uwanjani na kuzimia huku wachezaji wenzake wakimzinguka kwenye eneo la kona ya Galatasaray.
  Mwaka 2009 Gomis aligundulika kuwa na presha ya kushuka kiasi cha kuzimia. Mwaka huo, alizimia kwenya kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa na akazimia tena katika matukio mengine matatu.
  Mshambuliaji wa Galatasaray, Bafetimbi Gomis jana alizimia uwanjani katika mechi dhidi ya Kasimpasa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Kwa siku za karibuni, Gomis alizimia tena wakati bado anacheza Swansea katika mechi dhidi ya Tottenham mwaka 2015.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaweza kupoteza fahamu kwa muda, lakini kupatiwa huduma ya kwanza anaweza kuzinduka na kuendelea kucheza.
  Gomis amefunga mabao 20 kwenye mechi 26 alizoichezea Galatasaray kwenye mashindano yote tangu ajiunge nayo msimu uliopita. 
  Baada ya kujiunga na Swansea kutoka Marseille mwaka 2014, Gomis alifunga mabao 17 katika mechi 71 za mashindano yote za klabu huyo ya Wales. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BAFETIMBI GOMIS AZIMIA UWANJANI AKIICHEZEA GALATASARAY UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top