• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 23, 2018

  LIGI KUU YA WANAWAKE KUZINDULIWA RASMI NA WAZIRI MWAKYEMBE JUMAPILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inataraji kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma Jumapili Februari 25,2018 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
  Mchezo utakaotumiwa kuzindua ligi hiyo utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz ya Kigoma dhidi ya Simba ya Dar es Salaam.
  Aidha uzinduzi utaenda sanjari na mpango maalumu wa FIFA wa kuhamasisha soka la Wanawake uliopewa jina la Live Your Goal ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi ufunguzi wa Ligi ya Wanawake

  Mbali na mechi ya uzinduzi mechi nyingine za ligi hiyo ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite zinatarajia kuchezwa kesho kwenye viwanja tofauti.
  Uwanja wa Samora Panama FC watacheza dhidi ya Evergreen Queens ya Dar es Salaam saa 10 jioni,huko Mbweni JKT Queens watacheza dhidi ya Alliance saa 10 jioni,mabingwa watetezi Mlandizi Queens wanasafiri mpaka Jamhuri Dodoma kucheza na Baobab Queens.
  Wakati huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12 Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Ujiji,Kigoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI KUU YA WANAWAKE KUZINDULIWA RASMI NA WAZIRI MWAKYEMBE JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top