• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 27, 2018

  MAREFA WA AFRIKA KUSINI KUCHEZESHA SIMBA SC NA EL MASRY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
  Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
  Nyota wa Simba SC, Shiza Kichuya yuko vizuri kuelekea mechi na El Masry  
  Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea.
  Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA AFRIKA KUSINI KUCHEZESHA SIMBA SC NA EL MASRY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top