• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 21, 2018

  EL MASRY WATUA ANGA ZA SIMBA PAMOJA NA KUPIGWA ZAMBIA

  TIMU ya Green Buffaloes jana iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya El Masry Uwanja wa Nkoloma mjini Lusaka, lakini haukutosha kuwabakiza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Timu hiyo ya Zambia inatolewa kwa kipigo cha jumla cha 5-2, kufuatia kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza Februari 10, Uwanja wa Port Said.
  Mabao ya Buffaloes, waliorejea kwenye michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008 jana yalifungwa na mshambuliaji mkongwe, Felix Katongo dakika ya 11 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Mike Katiba na beki Stephen Kabamba dakika ya 86.
  Bao pekee la El Masry inayofundishwa na gwiji wa Misri, Hossan Hassan katika mchezo wa jana lilifungwa na Ahmed Gomaa dakika ya 16 aliyetumia makosa ya beki Malan Gondwe.
  Masry sasa watamenyana na Simba SC ya Tanzania iliyoitoa Gendarmerie Tnare ya Djibouti.

  Masry sasa watamenyana na Simba SC ya Tanzania iliyoitoa Gendarmerie Tnare ya Djibouti

  MATOKEO YOTE NA RATIBA KOMBE LA SHIRIKISHO
  Jana Februari 20, 2018
  Masters Security (Malawi) 0-0 Petro Atletico (Angola) (0-5)
  Cape Town City (Afrika Kusini) 1-0 Young Buffaloes (Swaziland) (1-0)
  Hafia (Guinea) vs Energie (Benin) (0-1)
  Anse Reunion (Shelisheli) 1-2 APR (Rwanda) (0-4)
  Port Louis (Mauritius) vs Ngazi Sport (Comoro) (1-1)
  Deportivo Niefang (Equatorial Guinea) 1-0 New Stars (Cameroon) (1-2)
  CS la Mancha (Kongo) vs Tanda (Ivory Coast) (0-0)
  CR Belouizdad (Algeria) vs Onze Createurs (Mali) (1-1)
  Green Buffaloes (Zambia) 2-1 El Masry (Misri) (0-4)
  Gendarmerie (Djibouti) 0-1 Simba (Tanzania) (0-4)
  Jumatano Februari 21, 2018
  Jwaneng (Botswana) vs Costa do Sol (Msumbiji) (0-1)
  FOSA Juniors (Madagascar) vs AFC Leopards (Kenya) (1-1)
  Maniema Union (DRC) vs Mangasport (Gabon) (1-0)
  Etoile Filante (Burkina Faso) vs Olympic Star (Burundi) (0-0)
  Hawks (Gambia) vs Akwa United (Nigeria) (2-1)
  Sahel (Niger) vs Al Ittihad (Libya) (0-1)
  CARA (Kongo) vs Asante Kotoko (Ghana) (0-1)
  Mbour Petite Cote (Senegal) vs RS Berkane (Morocco) (1-2)
  FC Nouadhibou (Mauritania) vs Africa Sports (Ivory Coast) (1-1)
  Wolaitta Dicha (Ethiopia) vs Zimamoto (Zanzibar) (1-1)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EL MASRY WATUA ANGA ZA SIMBA PAMOJA NA KUPIGWA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top