• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 22, 2018

  SIMBA, YANGA ZOTE KUANZIA NYUMBANI TENA MECHI ZIJAZO MICHUANO YA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Simba na Yanga wote wataanzia nyumbani mechi zao za Raundi ya Kwanza mwezi ujao.
  Katika kombe la Shirikisho, Simba SC wataikaribisha El Masry ya Misri kwa mchezo wa kwanza kati ya Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Machi 16 Uwanja wa Port Said mjini Cairo.
  Katika Ligi ya Mabingwa; Yanga SC wataikaribisha Township Rollers ya Botswana Machi 7 Uwanja wa Taifa, kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi 17.
  Simba SC wataikaribisha El Masry Machi 6 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam

  Simba SC wamefika hatua hii baada ya kuitoa Gendarmerie Tnare ya Djibouti kwa jumla ya mabao 5-0, wakishinda 4-0 Dar es Salaam na baadaye 1-0 mjini Djibouti City, wakati Yanga imeitoa Saint Louis Suns United ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 Tanzania na kutoa sare ya 1-1 jana mjini Mahe.
  El Masry inayofundishwa na gwiji wa soka wa Misri, Hossam Hassam iliitoa Green Bufalloes ya Zambia kwa jumla ya mabao 5-2, ikishinda 4-0 Cairo na kufungwa 2-1 Lusaka, wakati Township Rollers imeitoa El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 4-2, ikishinda 3-0 Botswana na kufungwa 2-1 Khartoum.
  Yanga SC watakuwa wenyeji wa Township Rollers Machi 7, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA, YANGA ZOTE KUANZIA NYUMBANI TENA MECHI ZIJAZO MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top