• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 23, 2018

  ARSENE WENGER AKABIDHIWA GATUSO 16 BORA EUROPA LEAGUE

  Kocha wa AC Milan, Gennaro Gattuso atakutana na Arsene Wenger wa Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  RATIBA KAMILI EUROPA LEAGUE HATUA YA 16 BORA

  Lazio v Dinamo Kiev
  RB Leipzig v Zenit St. Petersburg
  Atletico Madrid v Lokomotiv Moscow
  CSKA Moscow v Lyon
  Marseille v Athletic Bilbao
  Sporting Lisbon v Viktoria Plzen
  Borussia Dortmund v Red Bull Salzburg
  AC Milan v Arsenal
  Mechi za kwanza: Machi 8
  Marudiano: Machi 15 
  TIMU ya Arsenal itamenyana na AC Milan katika hatua ya 16 Bora ya Europa League.
  Kikosi cha Arsene Wenger kimefuzu hatua hiyo licha ya kufungwa 2-1 nyumbani na Ostersunds Alhamisi joini, kutokana na kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini.
  The Gunners ilikuwa timu ya mwisho kupangwa leo katia droo iliyofanyika mjini Nyon, Uswisi mchana wa leo, maana yake wataanzia uigenini. 
  Kwa upande wake, AC Milan wamefuzu hatua hii baada ya ushindi wa jumla wa 4-0 dhidi ya Ludogorets.
  Mechi ya kwanza Uwanja wa San Siro itafanyika Machi 8, wakati Milan itasafiri kwenda Uwanja wa Emirates wiki moja baadaye, Machi 15.  
  Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye michuano ya Ulaya, Arsenal walitolewa na AC Milan kwa kufungwa jumla ya mabao 4-3 katika Ligi ya Mabingwa msimu wa 2011-2012.
  Milan iko chini ya kocha Gennaro Gattuso, kiungo wake wa zamani amepewa ukocha licha ya uzoefu wake mdogo.
  Gattuso anakumbukwa kugombana na kocha Msaidzii wa Tottenham, Joe Jordan wakati timu hizo zilipomenyana katika Ligi ya Mabingwa  mwaka 2011.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENE WENGER AKABIDHIWA GATUSO 16 BORA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top