• HABARI MPYA

  Saturday, February 24, 2018

  RUVU SHOOTING YAZINDUA JEZI ZA MASHABIKI KWA SARE NA FRIENDS RANGERS MABATINI

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ruvu Shooting leo imezindua jezi mpya zitakazotumiwa na mashabiki wa timu hiyo, zikiuzwa ka bei ya shilingi elfu 20 kila moja.
  Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo kwenye makao makuu ya timu hiyo, Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, ikihudhuriwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happines Willium Seneda.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Happines ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Pwani aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, alisema kuwa, watahakikisha wanaweka nguvu zote kwa timu hiyo na kutatua changamoto zinazoikabili.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani Happyness William Seneda (kushoto) akimkabidhi jezi ya mashabiki wa Ruvu Shooting, Meneja Mkuu Msaidizi wa kampuni ya Hawaii Tanzania, Ahmed Suleiman baada ya kushinda mnada wa jezi hiyo
  Wachezaji wa Ruvu Shooting wakishuhudia uzinduzi wa jezi za mashabiki wa timu hiyo

  "Kwa maagizo niliyopewa na Mkuu wa Mkoa, anasema sasa tunahitaji kuwekeza nguvu zote kwa timu hii ambayo ndiyo wawakilishi pekee wa mkoa wa Pwani katika Ligi Kuu Bara," alisema Happiness.
  Kaimu Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Meja Michael James, aliwashukuru wadhamini wa timu hiyo Kampuni wa Hawaii kupitia bidhaa yake ya maziwa ya Cowbell na kusema kuwa wao ndio waliofanikisha kwa kiasi kikubwa hafla hiyo kutokana pia na udhamini wao kwa timu hiyo.
  "Wadhanimi wetu Cowbell wanatambua umuhimu wa maendeleo ya michezo hasa soka ndiyo sababu kuu ya kuendelea kutoa sapoti kubwa kwetu, sasa timu hii haipo tena mikononi mwa jeshi na badala yake imebadilishwa na kuwa mfumo wa Kampuni ikiitwa Ruvu Shooting Limited," alisema James.
  Nae kwa upande wake Msemaji wa Cowbell, Elisaria Ndeta, aliwashukuru Ruvu kwa kutambua umuhimu wao na kuomba kuendelea kufanya vema na kupata matokea mazuri katika Ligi ili iwe chachu ya wao kuendele kujivunia udhamini mwao.
  Katika hatua nyingine timu ya Ruvu leo imetoka sare ya bila kufungana na timu ya Friends Rangers ya Magomeni, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jioni kuhitimisha hafla hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAZINDUA JEZI ZA MASHABIKI KWA SARE NA FRIENDS RANGERS MABATINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top