• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 20, 2018

  MECHI YA NDANDA NA YANGA SASA KUCHEZWA MWISHO WA MWEZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO namba 152 wa mzunguko wa 19 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Yanga SC umepangiwa tarehe ya kuchezwa.
  Bodi ya Ligi imetaja tarehe hiyo baada ya awali mchezo tajwa kutokuwa umepangiwa tarehe kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu.
  Mchezo huo sasa utachezwa Jumatano Februari 28, 2018 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mkoani Mtwara.
  Timu zote tayari zimejulishwa kuhusu tarehe ya kuchezwa mchezo huo.
  Kutoka kushoto; Nyota wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na Mzalendo Pius Buswita

  Wakati huo huo: Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeongeza tiketi kwa Tanzania kwa ajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Urusi mwaka huu.
  Kwa shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu wa namna ya kupata tiketi hizo.
  Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018.
  Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA NDANDA NA YANGA SASA KUCHEZWA MWISHO WA MWEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top