• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 24, 2018

  LIVERPOOL YASHINDA 4-1 NA KUPAA HADI NAFASI YA PILI ENGLAND

  Sadio Mane akiruka juu kushangilia kwa mbwembwe baada ya kuifungia Liverpool bao la nne dakika ya 77 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya West Ham United leo Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya Wekundu hao yamefungwa na Emre Can dakika ya 29, Mohamed Salah dakika ya 51 na Roberto Firmino dakika ya 57, wakati la Wagonga Nyundo limefungwa na Michael Antonio dakika ya 59, Liverpool ikipanda hadi nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 28, ikiishusha Manchester United yenye pointi 56 za mechi 27, wote wakiwa nyuma ya Manchester City inayoongoza kwa pointi zake 72 za mechi 27 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YASHINDA 4-1 NA KUPAA HADI NAFASI YA PILI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top