• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 27, 2018

  WENGER SASA SAFARI IMEIVA ARSENAL, WA KUMRITHI WATAJWA

  KLABU ya Arsenal itaitathmini nafasi ya Arsene Wenger mwishoni mwa msimu — kukiwa na uwezekano wa kuhitimisha miaka 22 ya Mfaransa huyo.
  The Gunners tayari wamekwishaanza kuandaa orodha ya makocha wa kuwatathmini katika kumpata mbadala wa Wenger kama itaamua kuachana naye mwishoni mwa msimu.
  Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim, kocha wa Ujerumani, Joachim Low, kocha Mkuu wa Celtic, Brendan Rodgers na kocha wa Manchester City, Mikel Arteta ni miongoni mwa watu awali walioorodheshwa.
  Arsene Wenger anaweza kuhitimisha miaka yake 22 ya kufanya kazi Arsenal mwishoni mwa msimu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Vyanzo vinasema kwamba Wenger, ambaye nafasi yake iko hatarini baada ya kipigo cha Jumapili katika fainali ya Carabao Cup kutoka kwa Manchester City, atalazimika kupambana ili kumalizia miezi yake 12 ya mkataba wake.
  Lakini inavyoonekana sasa ndani ya Arsenal nguvu ya kumng'oa Wenger klabu hiyo ya Kaskazini mwa London mwishoni mwa msimu.
  Tathmini ya mwishoni mwa msimu ndio itabeba mustakabali wa Wenger kama apewe nafasi nyingine ya kubaki kwa msimu mwingine au aondolewe. Hii inamuacha apambane maswali magumu juu ya nini amevuna katika msimu hadi sasa.
  Zaidi itategemea kama ataiwezesha timu kupata nafasi ya kurejea kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu, ingawa hiyo bado haitatosha kuwa sababu ya kumbakiza. 
  Na safari ya kurejea kwenye michuano hiyo mikubwa ya Ulaya inaonekana kuwa ngumu, kwa sasa The Gunners wakizidiwa pointi 10 na Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya nne.
  Hivyo, nafasi nzuri zaidi ya Arsenal kurejea kwenye michuano hiyo kwa kushinda taji la UEFA Europa League, ingawa wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kumenyana na AC Milan katika raundi ijayo, hatua ya 16 Bora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WENGER SASA SAFARI IMEIVA ARSENAL, WA KUMRITHI WATAJWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top