• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 26, 2018

  SUGU AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI MITANO JELA KWA KUMKASHIFU RAIS MAGUFULI

  Na David Nyembe, MBEYA
  GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Osmund Mbilinyi, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini kw asasa, amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
  Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya na Hakimu Michael Mteite baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa upande wa mashitaka.
  Pamoja, Mbilinyi maarufu kwa jina la utani, Sugu, Mahakama hiyo pia imemuhukumu kifungo cha miezi sita, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelei (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwa kosa hilo.
  Joseph Mbilinyi 'Sugu' (kushoto) akiwasili na mke wake mahakamani leo kusikiliza kesi yake

  Wakili Peter Safari, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka mahakamani leo

  Washtakia hao wanashutumiwa kutenda kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha Rais Magufuli Desemba 31 katika viwanja wa Luanda Nzovwe wakati wakizungumza na wananchi.
  Miongoni mwa viongozi waliokuwepo mahakamani hapo leo ni Wakili Peter Safari, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Dar es Salaam, John Mnyika, Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka na viongozi wengine wa CHADEMA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUGU AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI MITANO JELA KWA KUMKASHIFU RAIS MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top