• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 23, 2018

  MCHEZO WA LIPULI NA NDANDA WASOGEZWA

  BODI ya Ligi (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 153 kati ya Lipuli na Ndanda uliokuwa uchezwe Ijumaa Machi 2, 2018 kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.
  Mchezo huo sasa umesogezwa mpaka Jumapili Machi 4, 2018 na utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora.
  Sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kuipa nafasi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara baada ya mchezo wao na Yanga ambao sasa umepangwa kuchezwa Jumatano Februari 28, 2018 kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona, Mtwara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MCHEZO WA LIPULI NA NDANDA WASOGEZWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top