• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 20, 2018

  MBAO FC, NJOMBE MJI WAKATA UTEPE 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION KESHO

  RATIBA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP
  Februari 21, 2018
  Njombe Mji vs Mbao FC Saa 10:00 jioni
  Februari 24, 2018
  Singida United v Polisi Tanzania Saa 10:00 jioni
  KMC v Azam FC Saa 1:00 usiku
  Februari 25, 2018
  Buseresere v Mtibwa Sugar Saa 8:00 mchana
  Ndanda FC v JKT Tanzania                    Saa 10:00 jioni
  Maji Maji  v Yanga SC Saa 10:00 jioni
  Februari 26, 2018
  Kiluvya United v Tanzania Prisons         Saa 8:00 mchana 
  Stand United v Dodoma FC Saa 10:00 jioni

  Kinara wa mabao Mbao FC, Habib Kiyombo anatarajiwa kuiongoza timu yake dhidi ya Ndanda kesho

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

  HATUA ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuanza kesho kwa mchezo mmoja tu kufanyika Uwanja wa Saba Saba mjini baina ya wenyeji, Njombe Mji FC na Mbao FC ya Mwanza,utakaoanza Saa 10:00.
  Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea Jumamosi Februari 24, wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku Azam Complex.
  Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.
  Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBAO FC, NJOMBE MJI WAKATA UTEPE 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top