• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 25, 2018

  JKT TANZANIA YAITUPA NJE NDANDA FC KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya JKT Tanzania imeingia Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Ally Ahmed Shiboli dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza aliyefunga kwa penalti baada ya shuti lake kumbabatiza mkononi Ibrahim Job wa Ndanda.
  Ndanda ya kocha Malale Hamisini ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Abdallah Waziri kutolewa kwa kadi nyekundu kufuaatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za kawaida.
  Ally Ahmed Shiboli mfungaji wa bao pekee la JKT Tanzania leo ikiilaza 1-0 Ndanda FC                            PICHA YA MAKTABA

  JKT Tanzania inaungana na Yanga SC, Mtibwa Sugar, Azam FC, Singida United na Njombe Mji FC kutinga Robo Fainali ya michuano na timu mbili zaidi zitapatikana kesho kutokana na mechi kati ya Kiluvya United na Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani kuanzia Saa 8:00 mchana na Stand United na Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAITUPA NJE NDANDA FC KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top