• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 24, 2018

  SALAH AFIKIA REKODI YA MABAO YA SUAREZ LIVERPOOL MAPEMAA

  MSHAMBULIAji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah ameendeleza mwanzo wake mzuri Liverpool baada ya leo kufikia rekodi ya mabao ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Luis Suarez ya kufunga mabao 31 kwa msimu.
  Kwa kufunga leo kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Anfield, sasa amefikia idadi ya mabao ambayo nyota wa Uruguay, Suarez alifunga katika msimu wake wa mwisho Liverpool, 2013-14.
  Suarez ambaye baada ya hapo alihamia Barcelona, alifunga mabao hayo 31 katika mechi 37, kama Salah msimu huu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amefikisha rekodi hiyo mapema zaidi ya Suarez kwa sababu Liverpool ya Salah inacheza mashindano zaidi, ikiwemo Ligi ya Mabingwa.

  Mohamed Salah leo amefikia rekodi ya mabao ya Luis Suarez Liverpool
   PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  LUIS SUAREZ'S RECORD IN 2013-14 

  Mechi alizocheza: 37
  Mabao aliyofunga: 31 
  Pasi za mabao: 14
  Nafasi alizotengeneza: 101 

  REKODI YA MOHAMED SALAH MSIMU HUU 

  Mechi alizocheza: 37
  Mabao aliyofunga: 31 
  Pasi za mabao: 9
  Nafasi alizotengeneza: 62 


  Luis Suarez anayechezea Barcelona kwa sasa, msimu wa 2013-2014 alifunga mabao 31 katika mechi 37 Liverpool
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAH AFIKIA REKODI YA MABAO YA SUAREZ LIVERPOOL MAPEMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top