• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 24, 2018

  SINGIDA UNITED YAIFUATA NJOMBE MJI FC ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Namfua, Singida.
  Mabao ya Singida katika mchezo wa leo yalifunga na beki Kennedy Wilson Juma dakika ya 70 na Tafadzwa Kutinyu dakika ya 77 baada ya kubanwa na wapinzani wao awali.
  Kwa ushindi huo, Singida United ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm inaungana na Njombe Mji FC ambayo ilikuwa ya kwanza kwenda Fainali Jumatano kwa kuwatoa Mbao FC kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1.
  Hatua ya 16 Bora ya ASFC itaendelea Saa 1:00 usiku leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya KMC na Azam FC. 
  Kesho Maji Maji wataikaribisha Yanga Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kuanzia Saa 10:00 jioni, baada ya Buseresere FC kumenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza kuanzia Saa 8:00 mchana na Saa 1:00 usiku, JKT Tanzania watamenyana na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
  Mechi za 16 Bora ya ASFC zitakamilishwa Jumatatu ya Februari 26, Kiluvya United wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani Saa 8:00 mchana na Stand United watakuwa wenyeji wa Dodoma FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAIFUATA NJOMBE MJI FC ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top