• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 26, 2018

  MASHABIKI WAMJERUHI KOCHA UWANJANI UGIRIKI, MECHI YAVUNJIKA

  Kocha wa Olympiacos, Oscar Garcia akiugulia maumivu huku amejishika usoni baada ya kupigwa na burungutu la karatasi usoni na kukimbizwa hospitali huku mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji dhidi ya wenyeji, PAOK Salonika ukivunjika Uwanja wa Toumbas mjini Thessaloniki. 
  Mashabiki wa PAOK Salonika waliendelea kupambana na Polisi nje ya Uwanja hadi saa mbili zaidi baada ya mechi kuvunjika. 
  Olympiacos inatarajiwa kuzawadiwa ushindi wa mezani wa 3-0, huku PAOK ikikabiliwa na adhabu ya kutozwa fainali ya hadi Pauni 79,000 na inaweza kuamriwa kucheza bila mashabiki.
  Adhabu hiyo itairudisha nyuma PAOK katika mbio za ubingwa, ikipunguza idadi ya pointi wanazowazidi Olympiacos waliopo nafasi ya tatu na sasa timu zote zitabaki na pointi 49.
  Pamoja na hayo, Olympiacos inakabiliwa na adhabu ya kupokwa pointi baada ya vurugu walizofanya katika mechi dhidi ya AEK Februari 4 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI WAMJERUHI KOCHA UWANJANI UGIRIKI, MECHI YAVUNJIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top