• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 21, 2018

  SIMBA SC NA MBAO FC MOTO KUWAKA UWANJA WA TAIFA JUMATATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba SC na Mbao FC utafanyika Jumatatu ya Februari 26, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mechi hiyo pamoja na ya Ndanda FC na Yanga haikwenda sambamba na mechi nyingine za mzunguko wa 19 za Ligi Kuu, kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi walikuwa wanakabiliwa na michuano ya Kombe la Shirikishola Soka Afrika.
  Yanga nao ambao mechi yao na Ndanda haikufanyika kwa sababu walikuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, watasafiri kwenda Mtwara Jumatano ijayo.
  Nyota wa Simba SC kutoka kushoto; Shiza Kichuya, John Bocco na Muzamil Yassim, timu yao itamenyana na Mbao FC Jumatatu yUwanja wa Taifa

  Bodi ya Ligi imetaja tarehe za mechi hizo ambazo ni Simba v Mbao Februari 26 na Ndanda v Yanga Februair 28.
  Simba SC wanarejea leo Dar es Salaam baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gendarmerie Tnare mjini Djibouti City katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
  Kwa ushindi huo uliotokana na bao la Mganda, Emmanuel Okwi Simba dakika ya 55, Simba inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1 baada ya ushindi mwingine 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Februari 11.
  Sasa Simba SC ya kocha Mfaransa Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Mohamed Aymen Hbibi ambaye ni mchua misuli na Muharami Mohamed, kocha wa makipa itakutana na El Masry ya Misri iliyoitoa Green Buffaloes ya Zambia kwa jumla ya mabao 5-2, ikishinda 4-0 Cairo na kufungwa 2-1 jana mjini Lusaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA MBAO FC MOTO KUWAKA UWANJA WA TAIFA JUMATATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top