• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 22, 2018

  TOWNSHIP ROLLERS WAITUPA NJE MERREIKH LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Township Rollers ya Botswana imefanikiwa kuingia Raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kufungwa 2-1 na wenyeji, El Merreikh mjini Khartoum nchini Sudan jana.
  Hiyo inatokana na mtaji wao mzuri wa ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa nyumbani siku 11 zilizopita na sasa Township Rollers wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2.
  Maana yake, Township Rollers watamenyana na Yanga SC ya Tanzania iliyoitoa Saint Louis Suns United ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na jana kutoa sare ya 1-1 mjini Victoria.
  El Hilal ya Sudanimesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 ikishinda 3-0 Kartoum Ijumaa baada ya kufungwa 1-0 na LISCR nchini Liberia wiki mbili zilizopita.

  Township Rollers ya Botswana itamenyana na Yanga SC ya Tanzania

  MATOKEO YOTE RAUNDI YA AWALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
  Jumanne Februari 20, 2018
  Williamsville AC (Ivory Coast) 1-0 Stade Malien (Mali) (1-1)
  Olympic de Bangui (CAR) 0-0 ES Setif (Algeria) (0-6)
  El Hilal (Sudan) 3-0 LISCR (Liberia) (0-1)
  Jumatano Februari 21, 2018
  KCCA (Uganda) 1-0 CNaPs Sport (Madagascar) (1-2)
  Mbabane Swallows (Swaziland) 1-3 Bantu (Lesotho) (4-2)
  Aduana (Ghana) 2-0 El Tahadi (Libya) (0-1)
  Mounana (Gabon) 2-0 RC Kadiogo (Burkina Faso) (0-1)
  MFM (Nigeria) 1-0 AS Real (Mali) (1-1)
  MC Alger (Algeria) 9-0 AS Otoho (Congo) (0-2)
  Horoya (Guinea) 0-0 AS FAN (Niger) (3-1)
  Makkassa (Misri) 0-0 Generation Foot (Senegal) (0-2)
  Saint Louis (Shelisheli) 1-1 Yanga SC (Tanzania) (0-1)
  El Merreikh (Sudan) 2-1 Township Rollers (Botswana) (0-3)
  Leones Vegatarianos (Equatorial Guinea) vs Gor Mahia (Kenya) (0-2)
  Esperance (Tunisia) vs Concorde (Mauritania) (1-1)
  Eding Sport (Cameroon) 0-1 Plateau United (Nigeria) (0-3)
  AS Port (Togo) vs AC Leopards (Congo) (1-2)
  Zesco (Zambia) 7-0 JKU (Zanzibar) (0-0)
  ASEC Mimosas (Ivory Coast) vs Buffles (Benin) (1-1)
  UD Songo (Msumbiji) 2-0 Ngaya (Comoros) (1-1)
  Be Forward (Malawi) vs AS Vita (DR Congo) (0-4)
  FC Platinum (Zimbabwe) 1-2 Primeiro de Agosto (Angola) (0-3)
  Pamplemousses (Mauritius) 1-0 Bidvest (Afrika Kusini) (0-2)
  Difaa El Jadida (Morocco) 10-0 Benfica (Guinea Bissau)
  Benfica (Guinea Bissau) 0-0 Difaa El Jadida (Morocco) (0-10)
  Lydia Academic (Burundi) 0-1 Rayon Sports (Rwanda) (1-1)
  Jumamosi Februari 24, 2018
  Armed Forces (Gambia) vs Zanaco (Zambia) (0-3)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TOWNSHIP ROLLERS WAITUPA NJE MERREIKH LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top