• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 28, 2018

  YANGA KUVUNJA MWIKO WA KUTOIFUNGA NDANDA FC NANGWANDA LEO?

  REKODI YA YANGA NA NDANDA FC
                       P W D L GF GA  GD Pts
  Ndanda FC 8 3 3 2 8    4     4 10
  Yanga SC 8 2 3 3 4     8  -4 7
  Jumamosi Septemba 23, 2017
  Yanga SC 1-0 Ndanda, Uhuru, Dar es Salaam
  Jumatano Desemba 28, 2016
  Yanga SC 4-0 Ndanda, Uhuru, Dar es Salaam
  Jumatano Septemba 7, 2016
  Ndanda 0-0 Yanga SC, Nangwanda Sijaona, Mtwara
  Jumapili Mei 14, 2016
  Ndanda 2-2 Yanga SC, Taifa, Dar es Salaam
  (Ndanda ilikuja Dar badala ya kucheza nyumbani, kwa 

  sababu Yanga walikuwa kwenye michuano ya Afrika)
  Jumapili Januari 17, 2016
  Yanga SC 1-0 Ndanda FC, Taifa, Dar es Salaam
  Jumamosi Septemba 9, 2015
  Ndanda 1-0 Yanga SC, Nangwanda Sijaona, Mtwara
  Jumamosi Mei 9, 2015
  Ndanda 1-0 Yanga SC, Nangwanda Sijaona, Mtwara
  Jumamosi Januari 31, 2015
  Yanga SC 0-0 Ndanda FC, Taifa, Dar es Salaam
  Yanga SC haijawahi kushinda mechi dhidi ya Ndanda Uwanja wa Nangwanda, Mtwara

  Na Mwandishi Wetu, MTWARA
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakiwa wageni wa Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.  
  Huo ni mchezo wa kiporo wa mzunguko wa 19, ambao Yanga ilishindwa kuucheza kutokana na kukabiliwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns United ya Shelisheli.
  Na baada ya kuvuka Raundi ya Awali kwa ushindi wa jumla wa 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 1-1 ugenini, Yanga inakuja kumalizia kiporo chake kabla ya kwenda kucheza mechi ya Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
  Lakini Yanga itateremka Uwanja wa Nangwanda jioni ya leo ikiwa kumbukumbu ya kutoshinda mechi nyumbani kwa Ndanda kati ya tatu zilizotangulia, wakifungwa mbili na sare moja.
  Kwa ujumla, katika Ligi Kuu Yanga imekutana na Ndanda mara nane tangu hiyo ipande msimu wa  2014/2015 – huku mabingwa hao watetezi, wakishinda mechi tatu, kufungwa mbili na sare tatu. 
  Yanga itajaribu kusaka ushindi wa kwanza leo Uwanja wa Nangwanda ikiwa inabakiliwa na wimbi la majeruhi na matatizo mengi ndani ya timu.
  Lakini hata Ndanda, hawapo katika ubora waliokuwa nao misimu miwili iliyopita, wakitoka kutolewa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kwenye Ligi Kuu kwenyewe wamevuna pointi 18 katika mechi 18 na wanalindwa na pointi tatu tu kuwa katika eneo la kushuka Daraja.
  Yanga SC wanahitaji sana ushindi kwenye mchezo wa leo kupunguza idadi ya pointi wanazozidiwa na vinara, Simba SC katika mbio za ubingwa.
  Wakiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 19, Simba SC wamesimama imara kileleni mwa Ligi Kuu, wakifuatiwa na mahasimu wao, Yanga pointi 27 za mechi 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA KUVUNJA MWIKO WA KUTOIFUNGA NDANDA FC NANGWANDA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top