• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 18, 2018

  MBEYA CITY YANG’ANG’ANIWA NYUMBANI, SARE 0-0 NA STAND UNITED SOKOINE

  TIMU ya Mbeya City imelazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Stand United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Sare hiyo inaifanya Mbeya City ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi 19 na kuendelea kukamata nafasi ya nane, wakati Stand inayofikisha pointi 20 inabaki nafasi ya 10 kutokana na wastani wake mdogo wa mabao. 
  Ligi Kuu inatarajiwa inatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi mbili, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Sokoine na Mtibwa Sugar wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YANG’ANG’ANIWA NYUMBANI, SARE 0-0 NA STAND UNITED SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top