• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 20, 2018

  MAN CITY YAPIGWA 1-0 NA WIGAN NA KUTOLEWA KOMBE LA FA

  BAO pekee la mshambuliaji Will Grigg lilitosha kuipa Wigan Athletic ushindi wa 1-0 dhidi ya vigogo Manchester City 1-0 katika mchezo wa Kombe la FA England hatua ya 16 Bora usiku wa jana Uwanja wa DW. 
  Grigg alifunga bao hilo dakika ya 79 kwa shuti baada ya kuuwahi mpira kufuatia makosa ya beki, Kyle Walker na kumchambua kipa Caludio Bravo.
  Kwa matokeo hayo, Man City inatolewa Kombe la FA baada ya raundi tano na Wigana inakwenda Robo Fainali ambako itakutana na Southampton.

  Mshambuliaji wa Mnchester City, Sergio Aguero akijaribu kujibu mashambulizi ya mashabiki wa Wigan baada ya mechi jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Katika mchezo huo ulioambatana na vurugu, refa  Anthony Taylor alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Fabian Delph wa Man City mwishoni mwa kipindi cha kwanza kwa kumchezea rafu Max Power.
  Makocha wa timu zote mbili, Pep Guardiola wa Man City na Paul Cook wa Wigan walikasirika baada ya kadi hiyo nyekundu na kujikuta wanatupiana maneno makali.
  Baadaye Guardiola akalazimika kumzuia mshambuliaji wake, Sergio Aguero asigombane na kocha huyo wa Wigan.
  Na baada ya mchezo huo, mashabiki wa Wigan walivamia uwanjani kushangilia na kufanya fujo ikiwemo mmoja wao kumpiga ngumi Aguero.
  Baada ya kupigwa, Aguero alimkimbiza shabiki huyo kabla ya beki wa Wigan, Cheyenne Dunkley, kocha wa City, Mikel Arteta na physio, Steven Lilley walikwenda kumzuia Muargentina huyo. 
  Wazi Man City itawafungulia mashitaka Wigan kwa kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani na kuhatarisha usalama wa wachezaji. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAPIGWA 1-0 NA WIGAN NA KUTOLEWA KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top