• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 27, 2018

  HERRERA WA MAN UNITED HATARINI KWENDA JELA MIAKA MINNE

  KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera anakabiliwa na mashitaka ya kiungo cha miaka minne jela nchini Hispania kwa tuhuma za kupanga matokeo katika La Liga.
  Waendesha mashitaka wa Hispania wamesema walitaka kifungo cha miaka miwili jela na kufungiwa kucheza soka kwa miaka sita kwa kiungo huyo na wachezaji wengine 35 katika kesi iliyofunguliwa tena Mahakama ya Valencia mapema mwezi huu.
  Kifungo cha miaka miwili jela kwa mara ya kwanza kwa Hispania huwa mtu hawekwi gerezani, maana yake ikiwa Herrera atashitakiwa kwa makosa ya rushwa mchezoni ataepuka jela.

  Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera yuko hatarini kwenda jela miaka minne kwa tuhuma za kupanga matokeo La Liga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Lakini Jumatatu, ikabainika kwamba wanasheria wa Ligi hiyo kubwa Hispania, ambao pia wamechukua hatua dhidi ya wachezaji waliohusishwa kwenye uchunguzi wa Mei mwaka 2011 kutokana na mechi baina ya timu ya zamani wa Herrera, Zaragoza na Levante, walitaka adhabu kubwa zaidi  ya wanasheria wa Serikali kama watakutwa na hatia ya rushwa.
  Magazeti yenye heshima yakiwemo la kila siku, Las Provincias yamesema kifungo cha miaka minne jela — kifungo cha kawaida kinachowezekana — ni sehemu ya mashitaka waliyofungua wanasheria wa La Liga katika Mahakama ya Maelekezo Namba Nane ya Valencia.
  Deportivo La Coruna, timu iliyoteremka Daraja kutokana na ushindi wa Zaragoza wa 2-1 ugenini dhidi ya Levante bado haijawasilisha mashitaka yake na vyanzo vilisema kwamba hawakuwa tayari kusema watafanya hivyo lini.
  Gazeti la Las Provincias limesema kwamba wanasheria wa La Liga pia wanataka faini kwa wachezaji ya Pauni Milioni 2.56 kwa kila mmoja, zaidi ya Milioni 1.7 zinazotakiwa na waendesha mashitaka wa Serikali kama watuhumiwa watakutwa na hatia.
  Wachezaji wengine wanaokabiliwa na tuhuma hizo mbali ya Herrera ni pamoja na nyota wa Atletico Madrid, Gabi, mshambuliaji wa zamani wa Middlesborough, Cristhian Stuani na Javi Venta, ambaye alimalizia soka yake Brentford.
  Kocha wa wakati huo wa Zaragoza, Javier Aguirre na mmiliki wa zamani, Agapito Iglesias wote wanachunguzwa.
  Tume ya Rushwa ya Hispania imesema katika kurasa zake 17 kwamba fedha walizolipwa wachezaji tisa wa Zaragoza akiwemo Herrera na klabu hiyo zilirejeshwa taslimu na zinaweza kuwa walikabidhiwa wachezaji wa Levante.
  Waendesha mashitaka wa Serikali wamesema walikubali kupoteza mechi hiyo ya Mei 21, mwaka 2011 na kuwasaidia wapinzani wao waepuke kushuka Daraja watakapopokea malipo ya Pauni 852,000.
  Herrera alisema mapema mwezi huu kwamba; "Kama nilivyosema mwaka 2014 suala hili lilipoibuka, sijafanya na sitafanya, chochote kupanga matokeo ya mchezo.
  "Ikiwa nitaitwa kujieleza popote, nitafurahi kuhudhuria kwa sababu dhamira yangu ni nzuri kabisa. Naipenda soka na ninaamini juu ya mchezo wa kiungwana - kote, ndani na nje ya Uwanja,".
  Watuhumiwa wengine wote nao wamekata kufanya uchafu wowote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HERRERA WA MAN UNITED HATARINI KWENDA JELA MIAKA MINNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top