• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2017

  UGANDA KUMENYANA NA MADAGASCAR MCHEZO WA KIRAFIKI

  MSHAMBULIAJI kipenzi cha wana Simba, Emmanuel Arnold Okwi Jumatano jioni anatarajiwa kuiongoza timu yake ya taifa ya Uganda, The Cranes katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Madagascar.
  Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mandela uliopo Namboole mjini Kampala na ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi dhidi ya Ghana Jumamosi.Kikosi cha wachezaji 23, akiwemo kiungo William Kizito Luwagga wa CSM Polithecnica ya Romia kipo kambini tangu Jumatatu katika hoteli ya Sky, Nalya.
  Emmanuel Okwi Jumatano jioni anatarajiwa kuiongoza Uganda katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Madagascar

  Wachezaji waliopo kambini ni makipa Benjamin Ochan na Ismail Watenga na wachezaji wa ndani; Nico Wadada,  Denis Iguma,  Savio Kabugo, Bernard Muwanga,  Isaac Muleme, Timothy Awanyi, Ivan Ntege,  Tom Masiko, Muzamir Mutyaba,  Tom Masiko,  Derrick Nsibambi,  Nelson Senkatuka, Isaac Isinde,  Joseph Ochaya, Godfrey Walusimbi, Hassan Wasswa, Tonny Mawejje, William Kizito Luwagga,  Emmanuel Okwi, Edrisa Lubega na Geofrey Serunkuma
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA KUMENYANA NA MADAGASCAR MCHEZO WA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top