• HABARI MPYA

  Saturday, September 02, 2017

  POGBA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED

  KIUNGO Paul Pogba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Manchester United, hivyo kuwa mchezaji bora wa kwanza wa mwezi kwa msimu huu wa 2017/2018 baada ya kazi nzuri mwezi uliopita.
  Zaidi ya mashabiki 160,000 wamempigia kura katika akaunti ya Twitter ya klabu na Pogba akafanikiwa kuwaangusha Nemanja Matic na Phil Jones kuchukua tuzo hiyo.
  Ulikuwa mwezi mgumu na wa kukumbukwa kwa Pogba, ambaye alifunga mabao mawili, akitoa pasi ya bao moja na kuwa Mchezaji Bora wa Mechi mara mbili kutokana na kuonyesha kiwango kizuri uwanjani akiisaidia timu yake kumaliza mwezi kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kubeba pointi zote katika mechi tatu za awali.
  Mfaransa huyo alifunga katika ushindi wa 4-0 dhidi ya West Ham United na Swansea City, akamsetia Anthony Martial kufunga dhidi ya Swans na soka yake nzuri ikamfanya atajwe  Mchezaji Bora wa Mechi Uwanja wa Liberty kabla ya kufunga tena na kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester Uwanja wa Old Trafford.
  Bao lake dhidi ya The Hammers katika wiki ya ufunguzi ya Ligi Kuu, limewekwa kwenye orodha ya mabao ya kipekee ya klabu, wakati bao lake dhidi ya Swansea limeshinda tuzo ya Bao Bora la Mwezi Agosti.
  Na Pogba mwenye umri wa miaka 24, anachukua tuzo hizo akitoka kushinda tuzo za Mchezaji Bora wa Msimu wa michuano ya Europa League baada ya kuisaidia United kutwaa ubingwa msimu uliopita wa 2016/2017. 
  Pogba pia alishinda tuzo ya mwezi wa mwisho wa msimu uliopita, Mei baada ya kazi nzuri ikiwemo kufunga bao bao katika Europa League dhidi ya Ajax mjini Stockholm, Sweden. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top