• HABARI MPYA

  Friday, September 15, 2017

  AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUPIGA 1-0 KAGERA SUGAR

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam usiku huu.
  Shujaa wa Azam leo amekuwa mshambuliaji mpya, Mbaraka Yussuf Abeid aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 44 akimalizia pasi ya kiungo anayeinukia vizuri Yahya Zayed kumchambua kipa mkongwe, Juma Kaseja.
  Ikumbukwe Mbaraka amejiunga na Azam FC msimu huu akitokea Kagera Sugar iliyomchukua Simba ya dar es Salaam na leo amemuumiza kocha wake wa zamani, Mecky Mexime kwa bao hilo pekee.
  Mbaraka Yussuf Abeid (kulia) akishangilia baada ya kufunga bao pekee la ushindi
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kutoa sare moja, hivyo kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ingawa inaweza kudumua kwa saa 24 tu kulingana na matokeo ya mechi za kesho.   
  Kagera Sugar inabaki na pointi moja baada ya mechi tatu, baada ya awali kufungwa 1-0 na Mbao FC kabla ya kutoa sare ya Ruvu Shooting mechi zote hizo zikichezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
  Pamoja na kufungwa leo, lakini Kagera Sugar ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo walishindwa kuzitumiavizuri.
  Kikosi cha Azam FC: Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Frank Domayo/Stephane Kingue dk87, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Yahaya Mohammed/Iddi Kipwagile dk33, Mbaraka Yusuph na Yahya Zayed/Bryson Raphael dk77.
  Kikosi cha Kagera Sugar: Juma Kaseja, Suleiman Mangoma, Adeyum Ahmed, Juma Shemvuni, Juma Nyoso, Uzoka Ugochukwu, Japhet Makarai, Ally Idd, Themi Felix/Venence Ludovick dk49, Amme Ally/Ally Ramadhani dk75, Omary Daga/Edward Christopher dk85.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUPIGA 1-0 KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top