• HABARI MPYA

    Thursday, October 01, 2015

    NEEMA NYINGINE HIYO LIGI KUU! TFF WASAINI MKATABA NA NHIF

    KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na mfuko wa huduma ya afya (NHIF) kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachezaji wa Ligi Kuu pamoja na viongozi wa benchi la ufundi.
    Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika katika hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar es salaam ambapo katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF Rehani Athumani walisaini kwa niaba ya pande hizo mbili.
    Mshambuliaji wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi (kushoto) akimtoka beki wa Mwadui FC, Joram Mgeveke katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hivi karibuni

    Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uwekaji sahihi mkataba huo, Mwesigwa amesema anaishukuru NHIF kwa kudhamini kutoa huduma ya afya kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi kwa vilabu vyote 16 vinavyoshiriki Ligi kuu ya Vodacom.
    Aidha Mwesigwa ameviomba vilabu vya Ligi Kuu nchini kutoa ushirikiano na watoa huduma ya afya kwa wachezaji na viongozi kutoka NHIF pindi watakapokuwa wanafika kwenye vilabu vyao kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
    Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani akiongea kwa niaba ya mfuko huo amesema wako tayari kufanya kazi na kutoa huduma ya afya kwa ngazi zote ikiwemo kwa timu za madaraja ya chini pia.
    TFF na NHIF zimeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa huduma ya afya kwa wachezaji kwa ligi kuu na viongozi wa benchi la ufundi, mkataba ambao unaeza kuongezwa kila unapomalizika.
    TFF kwa kupitia bodi ya ligi inavitaka vilabu vyote vya Ligi Kuu vitoe ushirikiano kwa wafanyakazi wa NHIF katika kurahisiha shughuli za usajili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa na nyaraka sahihi zikiwemo picha za wahusika katika muda sahihi.
    NHIF wanakuwa wadhamini watatu Ligi Kuu, baada ya wadhamini wakuu, kampuni ya huduma za simu za mkononi, Vodacom na Azam TV wenye haki ya kuonyesha moja kwa moja mechi za ligi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NEEMA NYINGINE HIYO LIGI KUU! TFF WASAINI MKATABA NA NHIF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top