• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2015

    UZEMBE WA TFF, TANZANIA NJE KUFUZU MICHUANO YA VIJANA AFRIKA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    RATIBA ya mechi za kufuzu kwa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 23 Afrika, mwaka 2015 mjini Dakar Senegal imetoka na kwa bahati mbaya Tanzania haimo.
    Mara tu baada ya kuipata ratiba hiyo, BIN ZUBEIRY ilianza kutafuta sababu kwa nini vijana wa Tanzania hawatashiriki michuano hiyo na kilichogundulika ni uzembe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Uchunguzi unaonyesha Tanzania ilitumiwa barua ya kuthibitisha kushiriki michuano hiyo mapema mwaka 2013 na wakambiwa tarehe ya mwisho kuthibitisha ni Oktoba 31 mwaka huu, lakini hawakufanya hivyo. 
    Vijana hawa wamekuwa wakiandaliwa kwa ajili ya kucheza michuano ya U23, lakini uzembe wa TFF unawakosesha fursa hiyo

    Hatimaye droo ya michuano hiyo imepangwa mjini Cairo na kutolewa leo, lakini Tanzania haimo kwa sababu tu ya uzembe wa TFF.
    Na Tanzania inakosa nafasi ya kucheza michuano hiyo, wakati ambao TFF imekuwa ‘bize’ na mpango wa soka ya vijana kupitia programu ya Maboresho.
    Ilikuwa ni fursa nzuri kwa vijana wanaong’ara Tanzania walio chini ya umri wa miaka 23 kwenda kuiwakilisha Tanzania katika michano hiyo, lakini uzembe wa TFF unawakosesha nafasi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UZEMBE WA TFF, TANZANIA NJE KUFUZU MICHUANO YA VIJANA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top