• HABARI MPYA

  Monday, December 08, 2014

  YANGA SC WAINGIA KAMBINI LEO LANDMARK HOTEL

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inaingia kambini leo, katika hoteli ya Landmark, eneo la Mbezi Beach kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC mwishoni mwa wiki.
  Simba na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe 2 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- huo ukiwa mchezo wa pili tangu kuanzishwa mechi hiyo mwaka jana.
  Simba SC ilishinda 3-1 Desemba mwaka jana katika mchezo huo unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo mbili, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Kilimanjaro Premium Lager.
  Kikosi cha Yanga SC ambacho juzi kiliifunga Express 1-0

  Yanga SC katika kuonyesha kwamba imepania kulipa kisasi, inapeleka ‘jeshi’ lake katia hoteli ya hadhi ya nyota tatu kuwaandaa wachezaji wake kisaikolojia.
  Juzi, timu hiyo ya kocha Mbrazi, Marcio Maximo ilicheza mechi ya kirafiki na kushinda 1-0 dhidi ya Express ‘Tai Wekundu’ ya Uganda, ambayo siku moja kabla ilitoa sare ya 0-0 na Simba SC.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI LEO LANDMARK HOTEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top