• HABARI MPYA

  Monday, December 08, 2014

  NYOTA DRC ATAMBA WATAFANYA MAAJABU AFCON 2015

  KIUNGO mkabaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Distel Zola (pichani kulia) anaamini timu yake ipo tayari kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Equatorial Guinea.
  Huku timu yake ikiwa imepangwa Kundi B pamoja na Zambia, Tunisia na Cape Verde, Zola anayechezea klabu ya Chateauroux ya Ligue 2 Ufaransa, amesema kwamba japokuwa wamepangwa kundi gumu, lakini watakwenda kupambana.
  "Kundi C na D lina timu kubwa kaka tukirejea taarifa za vyombo vya habari. Tupo kundi moja na Zambia, washindi wa mwaka 2012, na Cape Verde, ambao wanashiriki kwa mara ya pili mfululizo, hivyo tunatakiwa kujituma.
  "Mara nyingi, ni timu ambayo watu hawaitarajii ndiyo hufanya maajabu. Tuna matumaini ya kufanya maajabu kwenye mashindano haya. Tulilazimika kupambana na timu ngumu kama Cameroon na Ivory Coast ili kufuzu na tupo hapa. Tunakwenda kuhakikisha tuko tayari na kucheza mechi kwa mechi. Ni matumaini tutaingia kwenye raundi ya mtoano," amesema.
  DRC ilikuwa timu ya 16 kufuzu kwenye fainali hizo, kufuatia kupita kama mshindi wa tatu bora. Timu hiyo ilimaliza na pointi tisa na matokeo mazuri zaidi na ya kukumbukwa kwao katika mechi za kufuzu ni ushindi wa 4-3 ugenini dhidi ya Ivory Coast kwenye Kundi D.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA DRC ATAMBA WATAFANYA MAAJABU AFCON 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top