• HABARI MPYA

  Sunday, December 14, 2014

  WACHEZAJI WATATU ZAMBIA WAPATA AJALI WAKIENDA KAMBI YA AFCON, MULENGA AVUNJIKA MGUU

  Na Mwandishi Wetu, LUSAKA
  WACHEZAJI watatu wa timu ya taifa ya Zambia, Changwe Kalale wa Power Dynamos, Nyambe Mulenga wa Zesco United na Satchmo Chakawa wa Green Eagles wamepata ajali jana.
  Watatu hao walikuwa kwenye basi dogo wakielekea kwenye kambi ya Chipolopolo kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazoanza Januari 17, mwakani nchini Equatorial Guinea na basi lao likagongana na gari lingine eneo la Kabwe.
  Taarifa ya Chama cha Soka Zambia (FAZ) imesema kwamba wamesikitishwa na taarifa kwamba Mulenga amevunjika mguu. 
  Nyambwe Mulenga amevunnika mguu na hatakuwepo kwenye kikosi cha Zambia AFCON
  Nyambe Mulenga akijuliwa hali hospitali

  “Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kwamba dereva wa basi la Zesco United amefariki dunia katika ajali hiyo, kama ilivyokuwa kwa watu wengine watatu kwenye gari hilo," imesema taarifa katika tovuti ya FAZ.
  Beki, Nyambe Mulenga amevunjiika mguu wake wa kulia na yuko katika hali mbaya, wakati Changwe Kalale, aliyepewa lifti na Chakao Siachimo, aliyekwenda kwa mazungumzo wote wanaendelea vizuri kwa mujibu wa taarifa ya Zesco United.
  Mhasibu wa klabu hiyo, Lomuthunzi Mbeba, Ofisa Masoko, Fusya Bowa, Ofisa Utawala Frank Chitambala na Mjumbe wa Kamati, Peter Mutale wote wamepata majeraha na wanaendelea vizuri.
  Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya amethibitisha kwamba Meneja wa timu ya Zambia, Lusekelo Kamwambi na Msaidizi wake, Chintu Kampamba wote wamekwenda hospitali kuwajulia hali wachezaji hao.
  Kuumia kwa Mulenga wazi kunamuondoa kwenye kikosi cha Chipolopolo kitakachoshiriki michuano hiyo, ambayo Zambia imepangwa Kundi B na DRC, Cape Verde na Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WATATU ZAMBIA WAPATA AJALI WAKIENDA KAMBI YA AFCON, MULENGA AVUNJIKA MGUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top