• HABARI MPYA

  Sunday, December 14, 2014

  AZAM FC YALALA 3-2 KWA SC VILLA

  AZAM FC imefungwa mabao 3-2 na wenyeji SC Villa Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Uganda katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo.
  Azam FC ambayo imeweka kambi ya kujiandaa na hatua ijayo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika mchezo wa leo iliathiriwa na makosa na safu ya ulinzi na kukubali mabao hayo.
  Mabao ya Azam FC inayofundishwa na makocha Mcameroon, Joseph Marius Omog na Mganda George ‘Best’ Nsimbe, yamefungwa na  Didier Kavumbagu na Khamis Mcha Vialli.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Serge Wawa, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Mudathir Yahya, Didier Kavumbagu/Gaudence Mwaikimba, Amri Kiemba na Khamis Mcha ‘Vialli’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALALA 3-2 KWA SC VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top