• HABARI MPYA

  Monday, December 15, 2014

  YANGA SC YAMTEMA EMERSON, YAMSAJILI TAMBWE ALIYETEMWA SIMBA SC

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imemuacha Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mrundi Amisi Tambwe.
  Tambwe amesaini usiku huu Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachwa na klabu yake, Simba SC aliyoichezea msimu mmoja uliopita akitokea Vital’O ya Burundi.
  Yanga SC imeamua kumuacha Mbrazil Emerson baada ya kushindwa kupata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
  Tambwe anaungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni Yanga SC.
  Amisi Tambwe kushoto akisaini Mkataba wa Yanga SC pembeni ya Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Francis Kifukwe
  Tambwe akitia dole gumba kwenye fomu za Mkataba wa Yanga SC, pembeni ya Wakili Stoki Joachim kushoto 

  Wakati dirisha la usajili linafungwa Saa 6:00 usiku leo, Yanga SC imesajili jumla ya wachezaji watatu wapya baada ya kumuacha Emerson, mwingine ni Danny Mrwanda.  
  Katika kipindi cha msimu mmoja, Tambwe ameichezea Simba SC jumla ya mechi 43 na kuifungia mabao 26.
  Maisha yake yalianza kuwa magumu Simba SC baada ya ujio wa kocha Mzambia, Patrick Phiri kuchukua mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic.
  Emerson (katikati) ameichezea Yanga SC mechi moja tu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTEMA EMERSON, YAMSAJILI TAMBWE ALIYETEMWA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top