• HABARI MPYA

  Monday, December 15, 2014

  MAN CITY YAPEWA BARCA, CHELSEA NA PSG, REAL NA SCHALKE, ARSENAL NA MONACO

  MABINGWA wa England, Manchester City kwa mara nyingine tena watamenyana na Barcelona katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya droo iliyopangwa mjini Nyon leo.
  Tmu hiyo ya Katalunya, iliitoa timu ya Manuel Pellegrini katika hatua kama hiyo msimu uliopita kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1.
  Chelsea itamenyana na mabingwa wa Ligue 1, Paris Saint-Germain- maana yake itakutana na beki wake wa zamani, David Luiz.
  The Blues iliitoa timu hiyo ya Ufaransa katika Robo Fainali msimu uliopita kwa faida ya mabao ye ugenini, baada ya sare ya jujla ya 3-3, ikishinda 2-0 nyumbani na kufungwa 3-1 mjini Paris. 
  Wakati huo huo, Arsenal itamenyana na vigogo wengine wa Ufaransa, Monaco maana yake kocha Arsene Wenger atakitana na waajiri wake wa zamani.

  RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA 16 BORA... 

  Paris Saint-Germain vs Chelsea Manchester City vs Barcelona 
  Bayer Leverkusen vs Atletico Madrid
  Juventus vs Borussia Dortmund  
  Schalke 04 vs Real 
  Madrid 
  Shakhtar Donetsk vs 
  Bayern Munich 
  Arsenal vs Monaco
  Basle vs Porto 
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 17/18 na 24/25, wakati marudiano yatakuwa Machi 10/11 na 17/18.  
  The Champions League trophy on display at the last 16 draw in Nyon, Switzerland on Monday
  UEFA General Secretary Gianni Infantino pulls Manchester City out of the pot during the last 16 draw
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAPEWA BARCA, CHELSEA NA PSG, REAL NA SCHALKE, ARSENAL NA MONACO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top