• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR KUIVAA BURUNDI DESEMBA 9 TAIFA

  Kocha wa Stars, Mart Nooij
  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
  Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.
  Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
  Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.
  Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR KUIVAA BURUNDI DESEMBA 9 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top