• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  SERGE WAWA APAGAWA NA VIPAJI VYA AZAM AKADEMI, ARUDIA YALE YALE YA KING PELE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BEKI mpya wa Azam FC, Serge Wawa Pascal amesema akademi ya klabu hiyo ni ‘lulu’.
  Wawa aliyesajiliwa dirisha hili dogo kutoka El Merreikh ya Sudan amesema hayo baada ya Azam FC kucheza mchezo wa kirafiki na Azam Academy jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Azam FC walishinda 1-0, bao pekee la kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyetokea benchi kipindi cha pili kumpokea Amri Kiemba, lakini ukweli ni kwamba watoto waliwahenyesha kaka zao.
  Serge Wawa Pascal amesema vijana wa Azam Academy ni 'lulu' 

  “Tumecheza mechi moja nzuri sana na hawa watoto, wametupa changamoto nzuri, nimevutiwa na vipaji vya vijana niliowaona hapa, kuna nyota wengi wa baadaye wakubwa hapa,”amesema Wawa.
  Wawa amesema kwamba vijana wa Azam Academy wanajua soka na anaamini wengi wao watafika mbali, kama si kuchezea Azam kubwa basi hata klabu nyingine.
  “Katika hawa vijana, nadhani wapo ambao watacheza hadi Ulaya, kwa kweli wamenivutia sana na ninaomba timu nyingine hapa Tanzania ziige mfano huu,”amesema mchezaji huyo kutoka Ivory Coast.    
  Maneno kama hayo kuhusu akademi ya Azam FC, yamewahi kutolewa na Mwanasoka Bora wa zamani wa Afrika, Abedi Ayew Pele alipotembelea Chamazi miaka miwili iliyopita.
  Pele, Mghana aliyewika Marseille ya Ufaransa alitembelea Chamazi wakati wachezaji kama Aishi Manula, Gardiel Michael, Kevin Friday, Farid Mussa, Joseph Kimwaga, Mudathir Yahya na wengine wapo akademi, lakini wote hao sasa ni wachezaji wa Azam FC na timu ya taifa, Taifa Stars.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERGE WAWA APAGAWA NA VIPAJI VYA AZAM AKADEMI, ARUDIA YALE YALE YA KING PELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top