• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  ESPERANCE ‘WAMTIA PINGU’ KIPA WAO TEGEMEO

  Na Mwandishi Wetu, TUNIS
  VIGOGO wa Tunisia, Esperance wamefikia makubaliano na kipa wao, Moez Ben Cherifia (pichani kushoto) kuongeza Mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
  Ben Cherifia alianza soka yake na Esperance mwaka 2009 na sasa amekuw ammoja wa makipa bora nchini Tunisia.
  Kwa mujibu wa taarifa nchini Tunisia, wana Damu na Dhahabu hao wamefikia makubaliano na Ben Cherifia kuongeza Mkataba wake kwa misimu miwili zaidi, ambao utamfanya afanye kazi katika klabu hiyo hadi mwaka 2017.
  Mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Tunisia mwenye umri wa miaka 23, aliiongoza Esperance kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011 na ubingwa wa Ligi ya Tunisia msimu wa 2009/2010 na 2010/2011. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ESPERANCE ‘WAMTIA PINGU’ KIPA WAO TEGEMEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top