• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  STEPHEN BENGO AING'ARISHA SC VILLA

  Bengo akishangilia bao lake
  MKWAJU wa penalti wa Stephen Bengo kipindi cha kwanza umeipa pointi tatu SC Villa baada ya mabingwa hao mara 16 kuifunga Bright Stars 1-0 katika Ligi Kuu ya Uganda (UPL) viwanja vya Ssaza Grounds, Mityana jana.
  Huo unakuwa ushindi wa tisa katika mechi 14 kwa Villa, na kukifanya kikosi cha kocha Sam Ssimbwa kiindoe KCC katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, kwa kufikisha pointi 30, ikizidiwa moja tu na vinara, Vipers.
  Kipigo hicho kinakuwa cha nne kwa timu ya Fred Kajoba, Bright Stars msimu huu, ambacho kinawafanya washuke kwa nafasi moja hadi ya nane wakibaki na pointi zao 20.
  Wenyeji walipata bao la kuongoza dakika ya 17 baada ya mchezaji wa Villa kutoka Nigeria, Victor Emenayo kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari la Bengo akaenda kufunga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STEPHEN BENGO AING'ARISHA SC VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top