• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  SIMBA SC NA MWADUI YA JULIO JIONI YA LEO TAIFA

  SIMBA SC leo inacheza mchezo wa kirafiki na Mwadui ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa sababu kila timu imeuhitaji kwa sababu maalum.
  “Kama unavyojua, sisi tunajiandaa na Ligi Kuu, na wenzetu nao wanajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, ambako wanapigana kikamilifu ili kupanda, kwa hiyo itakuwa mechi tamu,”amesema Kaburu.

  Kiongozi huyo wa Simba SC amesema anatarajia kupata changamoto nzuri kutoka kwa Mwadui FC, inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
  Kaburu amesema Simba SC itashusha kikosi chake kamili kilichoichapa 2-0 Yanga SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe wiki iliyopita Uwanja huo huo, Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA MWADUI YA JULIO JIONI YA LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top