• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  URA YAICHAPA EXPRESS 1-0 LIGI KUU UGANDA

  URA wameng'ara jana Uganda
  BAO pekee la Frank Kalanda limeipa URA ushindi wa 1-0 dhidi ya Express katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uganda jana Uwanja wa Mehta mjini Lugazi.
  Ushindi huo unawafanya Watoza kodi hao washinde mechi ya saba na ya tatu mfululizo, hivyo kufikisha pointi 23 na kujikita nafasi ya nne.
  Kwa Tai Wekundu wanashuka kwa nafasi moja hadi ya saba wakibaki na pointi zao 21 baada ya mechi 14. Mchezo mwingine jana mabingwa watetezi, KCC wamefungwa 1-0 na Lweza Uwanja wa Wankulukuku.
  Entebbe nayo ilishinda mechi yake ya pili jana UPL baada ya kuwachapa Rwenshama 2-1 Uwanja wa Nakivubo. Ali Adam na Hussein Mubiru walifunga mabao ya Entebbe, wakati Farouk Kalinzi aliwafungia wageni la kufutia machozi.
  Mabao mawili ya Umar Kasumba yameipa ushindi wa 2-0 Polisi dhidi ya Soana Uwanja wa Kavumba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: URA YAICHAPA EXPRESS 1-0 LIGI KUU UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top