• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  STEPHEN APPIAH AIONYA GHANA, ASEMA WAKIFANYA MZAHA HAWAFIKI POPOTE

  Na Mwandishi Wetu, ACCRA
  NAHODHA  wa zamani wa Ghana, Stephen Appiah ameionya timu yake hiyo ya taifa, Black Stars kwamba ikifanya mzaha katika maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2015, haitafika popote.
  Baada ya droo iliyopangwa Jumatano iliyopita, timu hiyo kutoka Magharibi mwa Afrika imepangwa pamoja na Afrika Kusini, Algeria na Senegal.
  “Tuache kujidanganya wenyewe, hili ni kundi gumu mno, Tunaweza kutoka? Ndiyo. Tunatakiwa kujiandaa kwa ajili hiyo kuanzia mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal,”amesema.
  Stephen Appiah ameiasa Ghana ifanye maandalizi mazuri kuelekea AFCON

  Ametaka maandalizi ya mazuri yafanyike na mikakati thabiti iwekwe ili kikosi cha Ghana kiweze kusonga mbele kutoka kwenye kundi hilo linaloitwa la kifo.
  “Tuna fainali tatu tatu katika harua ya makundi. Ghana ina uwezo wa kufunga nchi yoyote duniani katika siku yetu, lakini wote tunatakiwa kufanya kazi makini sasa,” amesema.
  “Muda si rafiki kwetu, lakini acha tujiandae kikamilifu na tutafuzu,” amesema akizungumza na mtandao wa Ghanasoccernet. Michuano hiyo itafanyika nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17, mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STEPHEN APPIAH AIONYA GHANA, ASEMA WAKIFANYA MZAHA HAWAFIKI POPOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top