• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  YAYA TOURE ASEMA; AFCON 2015 HAINA MWENYEWE, MBAVU ZAKO TU

  Na Mwandishi Wetu, MANCHESTER
  MWANASOKA Bora wa Afrika, Yaya Toure, amesema kwamba hakuna timu ndogo tena Afrika na kuelekea Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea, mashindano yatakuwa magumu.
  Yaya ambaye timu yake, Ivory Coast imepangwa Kundi D pamoja na Cameroon, Guinea na Mali amesema soka ya Afrika sasa imekuwa na mashindano yatakuwa magumu mwakani.
  “AFCON hii inakwenda kuwa shindano moja ambalo hakuna timu inakwenda na uhakika wa kushinda."
  Yaya Toure amesema AFCON itakuwa ngumu mwakani

  “Hakuna timu ndogo tena Afrika. Kwa upande wetu tulikutana na timu ngumu kwenye kundi letu. Tunakwenda kwenye AFCON hii na kundi la wachezaji chipukizi wenye vipaji ambao ni matumaini yetu watajifunza kuwa washindi wazuri haraka iwezekanavyo."
  Pia amewashukuru Equatorial Guinea kuwa wenyeji wa mashindano hayo, kufuatia Morocco kujitoa kwa hofu ya ugonjwa wa ebola.
  Yaya ni mmoja wa Mabalozi wa Umoja wa Afrika katika vita dhidi ya ebola ambayo imeliathiri bara hili mwaka huu, ndani na nje ya Uwanja.
  Nahodha huyo wa Ivory Coast, anajiandaa kwenda kucheza Fainali za  Mataifa ya Afrika kwa mara ya sita tangu aanze kucheza soka ya kimataifa mwaka 2004.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAYA TOURE ASEMA; AFCON 2015 HAINA MWENYEWE, MBAVU ZAKO TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top