• HABARI MPYA

  Monday, December 15, 2014

  SOFAPAKA YAMNASA ADEBAYOR WA GOR MAHIA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  MABINGWA wa Ngao ya GOtv Sofapaka wamemsajili aliyekuwa mshambulizi wa Gor Mahia Kevin Omondi maarufu kama Adebayor au Ade kwa kifupi huku wakijiandaa kuakilisha taifa la Kenya katika michuano ya kuwania kombe la Confederations mwaka ujao.
  ‘Ade’ ametia mkataba wa miaka miwili na kusitisha juhudi zake za kusaka klabu baada ya uhamisho wake kuelekea klabu ya Afrika Kusini ya Moroka Swallows kutibuka kwa sababu zisizoeleweka.

  Mshambuliaji Kevin Omondi maarufu kama Adebayor ametua Sofapaka

  Omondi ni mchezaji mzuri na mwenye tajiriba ambaye tuna imani atatusaidia katika mechi za bara afrika mwaka ujao, rais wa Sofapaka na Mkongo Elly Kalekwa alithibitisha uhamisho huo akizungumza na mtandao wa futaa.com
  Kando na ‘Ade’ Sofapaka huenda wakamnasa pia straika chipukizi la Top Fry AllStars Erastus Mwaniki baada ya kumuonyesha mlango kiungo Anthony Kimani ambaye amejiunga na klabu ya Bandari kwa mkataba wa miaka miwili.
  Klabu hiyo ya pwani ya Kenya ilitoa kitita cha shilingi 450, 000 pesa za Kenya ili kumnasa Kimani. Kando na kiungo huyo, Bandari pia wamewasajili washambulizi George Abege kutoka Nairobi City Stars na John Ndirangu wa Top Fry AllStars pamoja na kungo Lawrence Kasadha (Nairobi City Stars). Abege na Kasadha ni raia wa Uganda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SOFAPAKA YAMNASA ADEBAYOR WA GOR MAHIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top