• HABARI MPYA

  Monday, December 08, 2014

  SIMBA SC WAPIGA NONDO, WATIMKIA ZENJI MAANDALIZI NANI MATANI JEMBE 2

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inaondoka jioni hii kwenda visiwa Zanzibar, kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Jumamosi.
  Baada ya kipigo cha mabao 4-2 jana kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Wekundu hao wa Msimbazi wanakwenda kurekebisha makosa Zanzibar.   
  Simba SC ilikuwa imeweka kambi Ndege Beacho Hotel, Kigamboni, Dar es Salaam, lakini baada ya mechi ya jana wameona bora wahamie Zanzibar.
  Dan Sserunkuma akiwa mazoezini na Simba SC gym leo kabla ya safari ya Zanzibar leo

  Lakini Zanzibar ndiyo sehemu ambayo mara nyingi Simba SC hupendelea kuweka kambi ya maandalizi ya msimu na hata kwa mechi za mahasimu wao hao, Yanga SC.
  Simba SC inapambana kutaka kulinda heshima ya ushindi wa 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe Desemba mwaka dhidi ya mahasimu hao wa jadi.
  Leo asubuhi, Wekundu hao wa Msimbazi walifanya mazoezi ya Gym Chang’ombe, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPIGA NONDO, WATIMKIA ZENJI MAANDALIZI NANI MATANI JEMBE 2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top