• HABARI MPYA

  Monday, December 08, 2014

  DANNY MRWANDA ASAINI MWAKA YANGA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Daniel ‘Danny’ Davis Mrwanda amesaini Mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga SC akitokea Polisi ya Morogoro.
  Mrwanda aliyewahi kuwika Simba SC amesaini Mkataba huo usiku huu na amesema mashabiki wa Yanga SC watarajie vitu vizuri.
  “Hii ni changamoto kwangu, kusaini klabu nyingine kubwa kama Yanga baada ya kucheza Simba SC wakati fulani, maana yake ninatakiwa kudhihirisha kitu,”amesema Mrwanda akizungumza na BIN ZUBEIRY mida hii.
  Mrwanda amesema kwamba Simba SC na Azam FC zote zilifanya naye mazungumzo, lakini hawakufikia makubaliano na baada ya Yanga SC kukidhi matakwa yake, anajitoa kuitumikia klabu hiyo.
  Danny Mrwanda akitia dole gumba fomu za Mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga SC usiku huu na picha za chini anasaini na akifurahia baada ya kusaini
   

  Mrwanda kutua Yanga SC ni kutimia kwa ndoto zake, kwani wakati anachipukia kisoka aliwahi kwenda kufanya majaribio ya kuomba kusajiliwa, lakini hakufanikiwa mwaka 2005 na karudi AFC ya Arusha.
  Mrwanda, mwenye umri wa miaka 31 sasa, aliibukia AFC ya mwaka mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2006 alipohamia Simba SC alikocheza hadi 2009 alipokwenda Al Tadamon ya Kuwait.
  Alirejea Simba SC mwaka 2009 na akacheza hadi 2010 alipokwenda Vietnam kujiunga na Dong Tam Long An ambayo aliichezea kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Hoang Anh Gia Lai aliyochezea hadi mwaka huu alipojiunga na Polisi Morogoro.
  Baada ya kusaini Mkataba huo, usiku huu Mrwanda anakwenda kujiunga na wachezaji wenzake katika hoteli ya Landmark, Mbeazi Beach kwa maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DANNY MRWANDA ASAINI MWAKA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top